PENTACHLORONAPHTHALENE ICSC: 0935
Machi 2001

CAS # 1321-64-8 C10H3Cl5
RTECS # QK0300000 Masi ya molekuli: 300.4
UN #
EC # 602-041-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Mnyunyizo wa maji, povu, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 21/22-36/38-50/53
S: (2-)-35-60-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PENTACHLORONAPHTHALENE ICSC: 0935
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO MANJANO ISIYOKOZA AU NYEUPE, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu ya kloridi hidrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): 0.5 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye mafusho na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi (chloracne). Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha kuharibika kwa ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 327-371°C
Kiwango myeyuko: 120°C
Uzito wiani: 1.7 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <0.1
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 10.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 8.73-9.13
DATA YA MAZINGIRA
Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye samaki. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Halowax ni jina la kibiashara ya naftalini za klorini.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005