1-OCTENE ICSC: 0934
Oktoba 2004

1-Octylene
1-Caprylene
Oct-1-ene
CAS # 111-66-0 C8H16 / CH3(CH2)5CH=CH2
RTECS # Masi ya molekuli: 112.2
UN # 1993
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda kavu. Povu. Dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kusinzia. Kizunguzungu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchangadry au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-I+II
Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Weka gizani. Baridi. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1-OCTENE ICSC: 0934
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia mpira, paints and lining materials.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Mfiduo wa viwango vya juu husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 123°C
Kiwango myeyuko: -102°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.7
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.0004
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.06
Kiwango cha kumweka: 10°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 256°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.7-3.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.5-4.6
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005