NITROGEN DIOXIDE ICSC: 0930
Mei 2003

Nitrogen peroxide
(silinda)
CAS # 10102-44-0 NO2
RTECS # QW9800000 Masi ya molekuli: 46.01
UN # 1067
EC # 007-002-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine.
Usigusishe na vinavyoweza kuwaka.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kutapika. Kukosa pumzi. Udhaifu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Ondoa mvuke kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Zimua maji yaliyotumika na chaki au magadi. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Alama: T+
R: 26-34
S: (1/2-)-9-26-28-36/37/39-45
Angalia: [5]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 5.1 na 8

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1067
Msimbo wa NFPA: H 3; F 0; R 0; OX
Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
NITROGEN DIOXIDE ICSC: 0930
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI NYEKUNDU-KAHAWIA AU KIOEVU KAHAWIA AU MANJANO CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka pamoja na maji kusababisha asidi nitriki na oksidi ya nitriki. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 3 ppm kama TWA, 5 ppm kama STEL, A4, (ACGIH 2003).
MAK: 5 ppm, 9.5 mg/m³. Aina ya kiwango cha juu: I (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye gesi au wenye mvuke kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa kinga mwili na mapafu kusababisha kupungua kwa uwezo wa mwili kujikinga dhidi ya magonjwa. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 21.2°C
Kiwango myeyuko: -11.2°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.45 (kioevu)
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 96
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.58
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Kioevu kinachouzwa cha rangi ya kahawia kilichowekwa kanieneo ni mchanganyiko ulio sawa wa dioksidi ya nitrojeni na tetroksidi ya nitrojeni isiyokuwa na rangi. Mkusanyiko usiowasha wa kemikali hii unaweza kusababisha mapafu kuvimba. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005