| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kutapika. Kizunguzungu. Degedege. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Kutapika. Kuhara. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombovinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Dutu hii ikiyeyuka: kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 21/22-36/38-50 S: (2-)-36/37-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT6-III
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO AU FUWELE NYEUPE YENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa inapogusana na asidi, vioksidishaji kuzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na bromidi hidrojeni, iodidi hidrojeni, oksidi za fosforasi. Dutu hii hutengana inapogusana na maji kuzalisha dichlorvos na dichloroacetaldehyde. Hushambulia metali, plastiki, mpira na mipako. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: (kiwango cha kunuswa) 0.1 mg/m³ kama TWA; (ngozi); A4; SEN; BEI imetolewa; (ACGIH 2005). MAK: being revised |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva kusababisha degedege, matatizo ya kupumua. Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kizuizi cha kolinesterasi; uwezekano wa madhara yake kulimbikizana: tazama athari za papo hapo/dalili. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 0.066kPa: 110°C Kiwango myeyuko: 26.5-27.5°C Uzito wiani (maji = 1): 1.96 katika 25°C Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 0.26 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 13.2 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.38 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa nyuki. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Tazama ICSC .
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||