| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Msongo/mfinyo (wa jicho), kukakamaa kwa msuli, utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kizunguzungu. Degedege. Kupoteza fahamu. Kutapika.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T+ R: 27/28 S: (1/2-)-23-28-36/37-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61 G43a
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho vioksidishaji vikali. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI AU MANJANO ISIYOKOZA HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile asidi fosforiki na oksidi za fosforasi. Humenyuka kwa ukali pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia feri, chuma cha pua, shaba nyeupe, aina fulani za plastiki, mpira na mipako. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.01 ppm; 0.092 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1997) TLV (kama STEL): 0.03 ppm; 0.27 mg/m³ (ACGIH 1997) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa nevakusababisha degedege, kutoweza kupumua. Kizuizi cha kolinesterasi. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 300°C Kiwango myeyuko: 6.9°C Uzito wiani (maji = 1): 1.25 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 21°C: 0.38 |
Kiwango cha kumweka: 79.5°C o.c. | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Apavinfos, Duraphos, Fosdrin, Gesfid, Phosdrin ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||