| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 48°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 48°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
|
Uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
|
Ainisho ya EU Alama: Xi, N R: 10-38-43-50/53 S: (2-)-24-37-60-61 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana pamoja na mchanganyiko wa iodini pentafloridi na tetrafloroethilini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); kuhisisha ngozi (Sh); (DFG 2004). |
HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera ngozi na inakera kwa upole macho. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi (tazama Vidokezo). | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 178°C Kiwango myeyuko: -74°C Uzito wiani (maji = 1): 0.84 Umumunyifu katika maji: katika 25°C ni dhaifu Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.19 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.7 |
Kiwango cha kumweka: 48°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 237°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 4.2 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Uhisishaji unaweza kutokea kwa dutu iliyooksidishwa. Hili linaweza kutokea kama dutu halisi au iliyozimuliwa ikiwa imehifadhiwa kwa siku kadhaa. UN 2052 (Kadi ya Usafirishaji wa Dharura 30S2052) na UN 2319 (Kadi ya Usafirishaji wa Dharura 30GF1-III) yenye daraja la 3 la Hatari, Kundi la Ufungashaji III hutumika katika usafirishaji wa dutu hii.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||