LEAD ARSENATE ICSC: 0911
Oktoba 1997

Arsenic acid, lead salt
Acid lead arsenate
Dibasic lead arsenate
CAS # 7784-40-9 PbHAsO4
RTECS # CG0980000 Masi ya molekuli: 347.1
UN # 1617
EC # 082-011-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Mipasuko ya misuli. Ukabidhi. Kuchangamka mno. Kuchanganyikiwa.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-61-62-23/25-33
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 221
Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 0;
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD ARSENATE ICSC: 0911
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA NYEUPE, NZITO, ISO HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 270° huzalisha mafusho yenye sumu kama vile arseniki, risasi na misombo yake.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama TWA): ppm; 0.15 mg/m³ as Pb_3(AsO_4)_2 (ACGIH 1997).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye vumbi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo na mfumo wa neva.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, mfumo wa neva, mafigo, ini na damu. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. Huweza kusababisha sumu inayoathiri uzazi kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): takribani 280°C
Uzito wiani (maji = 1): 5.79
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Hupatikana kiasili kama madini ya shultenite. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Gypsine na Soprabel ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005