LEAD ACETATE ICSC: 0910
Aprili 1997

Lead diacetate
Lead dibasic acetate
CAS # 301-04-2 C4H6O4Pb / (CH3COO)2Pb
RTECS # AI5250000 Masi ya molekuli: 325.3
UN # 1616
EC # 082-007-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Ukabidhi. Degedege. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 61-62-33-40-48/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 221
Kinachotenganishwa na brometi, carbonati, fosfeti na fenoli, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
LEAD ACETATE ICSC: 0910
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU PODA NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile oksidi risasi, asidi asetiki. Humenyuka vikali ikiwa na brometi, fosfeti, carbonati, fenoli.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Pb): ppm; 0.05 mg/m³ A3 (ACGIH 1996).
MAK: ppm; 0.1 mg/m³; kama Pb (1996).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka inaposambazwa, hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri damu na mfumo mkuu wa neva, kusababisha upungufu wa chembechembe nyekundu za damu, mvurugano wa neva, kuharibika kwa figo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, uboho, mfumo wa moyo na mishipa, mafigo, mfumo wa neva, kusababisha anemia, ongezeko la msukumo wa damu, kupooza, kuharibika kwa figo, madhara katika mwenendo. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Husababisha sumu kali inayoathiri uzazi kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 280°C
Uzito wiani (maji = 1): 3.3
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 44
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege, mamalia, udongo, maji. Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye mimea na wanyama. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za madhara ya sumu ya papo hapo hazijitokezi mpaka saa imepita.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005