| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
AFFF, poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kusinzia. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vya metali vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F R: 11-19 S: (2-)-9-16-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 128 Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 1; |
Isodhurika kwa moto. Baridi. Weka gizani. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kutengeneza peroksidi lipukaji kwa urahisi labda imezuiliwa, na kupasuka ikitikisa. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 250 ppm; 1040 mg/m³ ; STEL: 310 ppm; 1300 mg/m³ (ACGIH 1995-1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo zaidi ya OEL husababisha kupungua fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 69°C Kiwango myeyuko: -60°C Uzito wiani (maji = 1): 0.7 Umumunyifu katika maji: mbaya Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 15.9 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.5 Kiwango cha kumweka: -28°C Jotoridi la kujiwasha: 443°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-7.9 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kwa kawaida huwa na p-bentsiliaminofenoli kama kidhabitishi. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||