ISOBUTYRIC ACID ICSC: 0903
Machi 2002

2-Methylpropanoic acid
Dimethylacetic acid
Propionic acid, 2-methyl-
CAS # 79-31-2 C4H8O2 / (CH3)2CHCOOH
RTECS # NQ4375000 Masi ya molekuli: 88.11
UN # 2529
EC # 607-063-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu linalokinza alkoholi poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 56°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 56°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Maumivu. Wekundu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Osha kioevu kilichomwagika kwa maji mengi.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 21/22
S: (2)
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFC
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na besi kali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ISOBUTYRIC ACID ICSC: 0903
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni asidi dhaifu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 152-155°C
Kiwango myeyuko: -47°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.95
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 20
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 14,7°C: 0.13
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0
Kiwango cha kumweka: 56°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 481°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2-9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.88
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005