| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
(Tazama Kumeza).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xn, N R: 22-36/38-43-48/22-50 S: (2-)-22-24-37-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC2-II+III
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji, nitrati, nitriti na dutu za kuwaka.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE AU PODA NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho babuzi ya oksidi za sulfuri. Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati. Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji poda ya metali, nitrati, nitriti na chumvi za metali nzito. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha anemia. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko (hutengana): 120°C Uzito wiani: 1.88 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 58.7 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -3.6 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||