GRAFITI (ASILI) ICSC: 0893
Oktoba 1997

Plumbago
Black lead
Mineral carbon
CAS # 7782-42-5 C
RTECS # MD9659600 Masi ya atomi: 12.01
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ukwaru.
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza

Sukutua kinywa. Kupumzika.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kisha osha kwa maji mengi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
GRAFITI (ASILI) ICSC: 0893
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MAGAMBA, MABONGE, PODA, VIPANDE NYEUSI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka ikiwa na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: ppm; 2.0 mg/m³ sehemu pumuzi wa vumbi (ACGIH 1996-1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu yenye vumbi yake, kusababisha ugonjwa wa mapafu utokanao na grafiti (graphite pneumoconiosis).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango usablimishaji: 3652°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.09-2.23
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Tazama grafiti itengenezwayo CAS 7440-44-0. Itengenezwayo na ile ya asili zaweza kuchanganyiwa; na mazao mengi ya grafiti yana viongezeo vingine kama vile kristobaliti, tope la mkaa, na mafuta ya kipetroli. Kwa kawaida, kiasili grafiti huambatana na kiasi kidogo cha ulanga, oksidi feri, graniti na silika huru. Kiasi hicho ni kati ya 2-25%.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005