ETHYL n-BUTYL KETONE ICSC: 0889
Machi 1996

3-Heptanone
Butyl ethyl ketone
CAS # 106-35-4 C7H14O / CH3(CH2)3COCH2CH3
RTECS # MJ5250000 Masi ya molekuli: 114.21
UN # 1224
EC # 606-003-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 46°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 46°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vya metali vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A cha mvuke kikaboni).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-20-36
S: (2-)-24
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G35
Msimbo wa NFPA : H 1; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYL n-BUTYL KETONE ICSC: 0889
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm; 234 mg/m³ (ACGIH 1995-1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 147°C
Kiwango myeyuko: -39°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 187
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 46°C o.c.
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005