EDTA ICSC: 0886
Aprili 1997

N,N'-1,2-Ethanediylbis(N-carboxymethyl)-glycine
Ethylenediaminetetraacetic acid
Edetic acid
CAS # 60-00-4 C10H16N2O8 / ((HOOCCH2)2NCH2)2
RTECS # AH4025000 Masi ya molekuli: 292.2
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa (iwapo si poda).
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, shaba na aloi zake, nikeli.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
EDTA ICSC: 0886
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE AU PODA NYEUPE

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, besi kali, shaba na aloi zake, na nikeli.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mafigo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 150°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.086
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 0.05
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Trilon, Titriplex, Versene acid ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005