DINOCAP (ISOMER MIXTURE) ICSC: 0881
Oktoba 1997

2,4-Dinitro-6-(2-octyl)phenyl crotonate
2-Butenoic acid, 2(or 4)-isooctyl-4,6(or 2,6)dinitrophenyl ester
2,6(or 2,4)-Dinitro-4(or 6)octylphenyl crotonates in which octyl is a mixture of 1-methylheptyl, 1-ethylhexyl and 1-propylpentyl groups
DPC
CAS # 39300-45-3 C18H24N2O6
RTECS # GQ5775000 Masi ya molekuli: 364.4
UN #
EC # 609-023-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi Kupumua kwa shida. (Tazama Kumeza).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-38
S: (2-)-37
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DINOCAP (ISOMER MIXTURE) ICSC: 0881
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KAHAWIA ILIYOKOZA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 32°C.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera ngozi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii inaweza kusababisha ulemavu kwa watoto wa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko ifikapo 0.007kPa: 138-140°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.10
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Kinachotengenishwa na mafuta, mnyunyuzio utokanao na mafuta na mchanganyiko wa chokaa-sulfuri. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Caprane, Crotothane na Karathane ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005