| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na vinakisishaji.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na dutu za kuwaka na vinakisishaji.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa koo. Tazama Vidokezo.
|
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Tazama Ngozi.
|
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu.
|
Chombo maalum kisichopitisha joto. Ainisho ya EU Alama: O R: 8 S: (2-)-17 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2 Jasara tanzu za UN: 5.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 119 Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 0; OX |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU. KIOEVU BARIDI MNO KISICHO RANGI HADI BLUU HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki MAK haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii katika ukolezi mkubwa inakera njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -183°C Kiwango myeyuko: -218.4°C Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 20°C: 3.1 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo -118°C: 5080 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.43 |
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.65 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Nguo za kazi zilizoloweshwa kwa oksijeni huwa hatari kwa moto. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu. Dalili ya kuvuta hii gesi hutokea tu ukivuta nyingi zaidi. Pia shauriana na ICSC #0138 Oksijeni.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||