2,4,5-TRICHLOROPHENOL ICSC: 0879
Machi 1998

2,4,5-TCP
1-Hydroxy-2,4,5-trichlorobenzene
CAS # 95-95-4 C6H3Cl3O / C6H2Cl3(OH)
RTECS # SN1400000 Masi ya molekuli: 197.5
UN # 2020
EC # 604-017-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji vikali.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kutapika. Udhaifu. Kutokwa jasho.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio A/P2 cha mvuke kikaboni na vumbi linalodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-36/38-50/53
S: (2-)-26-28-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 804
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4,5-TRICHLOROPHENOL ICSC: 0879
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI AU MAGAMBA KIJIVUYENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kulipuka wakati wa kukanza hadi mtengano. Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapogusana na vioksidishaji vikali huzalisha mafusho yenye sumu na yakerayo (klorini, asidi hidrokloriki). Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka kwa alkali kwa joto ya juu ukitoa sumu kali ya dioksini ya klorini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. (Tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 253°C
Kiwango myeyuko: 67°C
Uzito wiani: 1.68 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.1
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 2.9
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.7
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Mazao ya kitekinikali yaweza kuwa na kiasi kidogo cha kemikali zenye sumu (dioksini za di-benzo poliklorini na furani za di-benzo poliklorini). Dutu hii inaweza kuwaka lakini kiwango mlipuko hakikuelezwa katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Caswell No. 879, Collunosol, Dowicide 2, NCI-C61187, Nurelle, Preventol I ni majina ya kibiashara. Ona ICSC 0588 2,3,4-trichlorophenol, ICSC 0589 2,3,5-trichlorophenol, ICSC 0590 2,3,6-trichlorophenol and ICSC 1122 2,4,6-trichlorophenol.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005