N,N-DIMETHYLANILINE ICSC: 0877
Machi 1998

N,N-Dimethylphenylamine
CAS # 121-69-7 C8H11N / C6H5N(CH3)2
RTECS # BX4725000 Masi ya molekuli: 121.2
UN # 2253
EC # 612-016-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 62°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 62°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Kutapika. Ulio kwa masikio. Kutoona vizuri.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vya metali au kioo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni). Vazi linalokinga kemikali.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-40-51/53
S: (1/2-)-28-36/37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 846-2
Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
N,N-DIMETHYLANILINE ICSC: 0877
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu sana (anilini, oksidi za nitrojeni). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm; 25 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1997)
TLV (kama STEL): 10 ppm; 50 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo juu zaidi ya OEL husababisha kupungua fahamu. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 192-194°C
Kiwango myeyuko: 2.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.96
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 67
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.2
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.002
Kiwango cha kumweka: 62°C
Jotoridi la kujiwasha: 371°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1-7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005