| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi.
|
Uingizaji hewa.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vya metali (chuma cha pua kinachopindika bila kukatika) vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
|
Ainisho ya EU Alama: F R: 11 S: (2-)-9-16-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G30 Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia plastiki nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 200 ppm; 705 mg/m³ (ACGIH 1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 102°C Kiwango myeyuko: -42°C Uzito wiani (maji = 1): (25°C) 0.81 Umumunyifu katika maji: wastani Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.0 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01 Kiwango cha kumweka: 13°C o.c. Jotoridi la kujiwasha: 452°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.6-3 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.99 (imekadiriwa) | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||