DIALLYLAMINE ICSC: 0866
Novemba 1998

Di-2-propenylamine
N-2-propenyl-2-propen-1-amine
CAS # 124-02-7 C6H11N / (CH2=CHCH2)2NH
RTECS # UC6650000 Masi ya molekuli: 97.2
UN # 2359
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kikohozi.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 6.1 na 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30G33
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIALLYLAMINE ICSC: 0866
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Mmumunyo huu katika maji ni besi kali ya kati. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na pamoja na asidi na vioksidishaji. Hushambulia shaba, bati, alumini na zinki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 112°C
Kiwango myeyuko: -88.4°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.76
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 9
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: takribani 2.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.06
Kiwango cha kumweka: 21°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.08
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005