HAFNIUM POWDER ICSC: 0847
Oktoba 1995

(poda)
CAS # 7440-58-6 Hf
RTECS # MG4600000 Masi ya atomi: 178.5
UN # 2545 (poda, kavu); 1326 (poda iliyonyunyishwa maji)
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda maalum.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani. Hatari ya moto na mlipuko (tazama Hatari za Kikemikali).
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko. Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Epuka kuvuta pumzi yenye vumbi laini au ukungu. Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.

Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama.

Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Loanisha poda kwa maji kwanza ili kuzuia vumbi na kushika moto, halafu kusanya poda na uweke kwa vyombo vilivyofunikwa vzuri. Kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2 (kavu); 4.1 (iliyonyunyishwa maji)

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41G13
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, halojeni, fosforasi na sulfuri. Weka chini ya maji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
HAFNIUM POWDER ICSC: 0847
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA KIJIVU

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa; katika joto la juu pamoja na nitrojeni, fosforasi na sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi kali, vioksidishaji vikali, halojeni kusababisha athari ya mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu. Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 4602°C
Kiwango myeyuko: 2227°C
Uzito wiani (maji = 1): 13.31
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Poda kwa kawaida huwekwa maji kiasi cha 25% ilikupungusa uwezo wa kupasuka. Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005