p-NITROCHLOROBENZENE ICSC: 0846
Oktoba 1997

1-Chloro-4-nitrobenzene
PCNB
PNCB
CAS # 100-00-5 NO2C6H4Cl
RTECS # CZ1050000 Masi ya molekuli: 157.6
UN # 1578
EC # 610-005-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).

Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!).
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/24/25-33
S: (1/2-)-28-37-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 877
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 2;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
p-NITROCHLOROBENZENE ICSC: 0846
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha gesi zenye sumu (oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni, fosjini na klorini). Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm; 0.64 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 242°C
Kiwango myeyuko: 82-84°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.3
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 30°C: 20
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.44
Kiwango cha kumweka: 127°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 510°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.39
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005