CAMPHECHLOR ICSC: 0843
Aprili 1997

Toxaphene
Chlorinated camphene (60%)
Polychlorocamphene
CAS # 8001-35-2 (karibu sawa na) C10H10Cl8
RTECS # XW5250000 Masi ya molekuli: 413.8 (katikati)
UN # 2761
EC # 602-044-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Povu, poda kavu, dioksidi kaboni, USITUMIE maji.
MLIPUKO Madhara ya mlipuko yanategemea kimumunyisho kilichotumika katika utengezaji.

Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama. Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Degedege. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/24/25-36/38
S: (2-)-13-44
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G53b
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CAMPHECHLOR ICSC: 0843
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO MANJANO KAMA NTA YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa, inapochomwa na/au inapoathiriwa na alkali, miale yenye nguvu na vichocheo vya metali, kama feri huzalisha mafusho yenye sumu. Hushambulia chuma. Haipatani na kiuadudu ya alkali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 mg/m³ (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1997)
TLV (kama STEL): 1 mg/m³ (ngozi) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha tetemeko na degedege. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 65-90°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.65
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 53
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 14.3
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini, viumbe vya ardhini, na ndege. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea viumbe vya majini.
VIDOKEZO
Hutengana ikikaribia kuchemuka. Camphechlor ni mchanganyiko wa kamfeni za klorini, ina klorini 67-69%. Kutumika kwa kiuadudu ya faa isitumike isipokuwa kama hakuna lingine. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Alltox, Chem-Phene, M 5055, Clor Chem T-590, Crestoxo, Estonox, Fasco-Terpene, Geniphene, Gy-phene, Hercules 3956, Melipex, Penphene, Phenacide, Phenatox, Strobane-T, Toxakil, Toxyphene, Toxon 63 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005