tert-BUTYL HYDROPEROXIDE (70 % AQUEOUS SOLUTION) ICSC: 0842
Oktoba 1999

1,1-Dimethylethylhydroxiperoxide
2-Hydroperoxy-2-methylpropane
CAS # 75-91-2 C4H10O2/(CH3)3COOH
RTECS # EQ4900000 Masi ya molekuli: 90.1
UN # 3109
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na dutu ziwakazo.
Mchanga mkavu, poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 43°C. Hatari ya moto na mlipuko inapokanzwa.
Mfumo funge wa zaidi ya 43°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Maumivu. Wekundu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Mchomo. Udhaifu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 5.2
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 839
Msimbo wa NFPA : H 1; F 4; R 4; ox
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi. Baridi. Chunguza mara kwa mara ili ugundue uvimbe na uvujaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
tert-BUTYL HYDROPEROXIDE (70 % AQUEOUS SOLUTION) ICSC: 0842
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi, misombo yenye sulfuri na metali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi, njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 89°C
Kiwango myeyuko: -3°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.93
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 3.07 imekadiriwa
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.1
Kiwango cha kumweka: 43°C
Jotoridi la kujiwasha: 238°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5-10
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.3 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Nambari ya UN (vimumunyishaji vinginezo kuliko ya maji): 3105. TBHP-70 na Trigonox A-75 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005