| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 71°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 71°C, uingizaji hewa.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kusinzia. Kichefuchefu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo kooni na kifuani. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
|
Ainisho ya EU Alama: Xn R: 20/21 S: (2-)-24 Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, na besi kali. Baridi. Weka gizani.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. na besi kali, kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 20 ppm kama TWA; A3; (ACGIH 2003). MAK: 20 ppm, 130 mg/m³, H; Aina ya kiwango cha juu: II(4); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2003). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu ya OEL huweza kusababisha kupoteza fahamu. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha vidonda vya seli za damu na kuharibika kwa figo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha anemia na kuharibika kwa figo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 192°C Kiwango myeyuko: -64°C Uzito wiani (maji = 1): 0.94 Umumunyifu katika maji: wastani (1.7 g/100 ml ifikapo 20°C) Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 31 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00 Kiwango cha kumweka: 71°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 340°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.9 (93°C) - 8.5 (135°C) Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.51 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||