BROMOTRIFLUOROMETHANE ICSC: 0837
Machi 1998

Trifluorobromomethane
Fluorocarbon-1301
Bromofluoroform
(silinda)
CAS # 75-63-8 CBrF3
RTECS # PA5425000 Masi ya molekuli: 148.9
UN # 1009
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Tazama Ngozi.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.2

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 644.
Isodhurika kwa moto iwapo ndani ya jengo. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BROMOTRIFLUOROMETHANE ICSC: 0837
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA ISO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho yenye sumu kama vile bromidi hidrojeni na floridi hidrojeni. Hushambulia plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1000 ppm; 6090 mg/m³ kama TWA (ACGIH 1997) MAK: 1000 ppm; 6100 mg/m³ IV (1995)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -58°C
Kiwango myeyuko: -168°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.5
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1434
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.86
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa tabaka ya ozoni.
VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Flugex 13B1, Freon 13B1, Halon 1301, Khladon 13B1 na Refrigerant 13B1 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005