BINAPACRYL ICSC: 0835
Aprili 1997

2-(1-Methylpropyl)-4,6-dinitrophenyl 3-methyl-2-butenoate
2-(1-Methylpropyl)-4,6-dinitrophenyl 3,3-dimethylacrylate
Dinoseb methacrylate
CAS # 485-31-4 C15H18N2O6
RTECS # GQ5600000 Masi ya molekuli: 322.3
UN # 2779
EC # 609-024-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto). Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kuumwa kichwa. Kutokwa jasho. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kutapika. Udhaifu.
Mtambo wa kutolea nje.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi kikali cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 61-21/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G41c
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BINAPACRYL ICSC: 0835
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa taratibu pamoja na maji kufanyiza Dinoseb.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri kimetaboliki, kusababisha joto la juu la mwili na kutokwa jasho. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 66-67°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 60°C: 0.013
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Binapacryl ni esta dimethilakriliki ya Dinoseb; humetabiliwa kufanyiza Dinoseb; sumu inasababishwa na Dinoseb. Tumia njia zote zinazowezekana kuzuia kushuka joto la mwili. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Acricid, Ambox, Endosan, Morocide, Niagara 9044 ni majina ya kibiashara. Pia shauriana na ICSC #0149 (Dinoseb) na ICSC # 0882 (Dinoseb acetate).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005