DI-n-HEPTYL PHTHALATE ICSC: 0832
Novemba 2003

1,2-Benzenedicarboxylic acid
Phthalic acid, diheptyl ester
Diheptyl phthalate
CAS # 3648-21-3 C22H34O4
RTECS # TI1090000 Masi ya molekuli: 362.51
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizio wa maji, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO


Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI


IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DI-n-HEPTYL PHTHALATE ICSC: 0832
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI AU HARUFU

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yakerayo.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 360°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.99
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.0002
Kiwango cha kumweka: 224°C c.c.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 7.6 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu kwa hiyo kunahitajika uangalifu mkubwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005