BARIUM SULFATE ICSC: 0827
Oktoba 1999

Barium sulphate
Blanc fixe
Artificial barite
CAS # 7727-43-7 BaSO4
RTECS # CR0600000 Masi ya molekuli: 233.43
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P1 cha chembe ajizi).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI


IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BARIUM SULFATE ICSC: 0827
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU FUWELE ISO HARUFU; ISO LADHA, NYEUPE AU MANJANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka kwa ukali sana pamoja na poda ya alumini.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 mg/m³ (ACGIH 1999).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa chembe za vumbi, kusababisha baritosis (ugonjwa wa mapafu unaotokana na bari).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 1600°C
Uzito wiani: 4.5 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Hupatikana kwa maumbile kama madini ya baraiti; jiwe ngumu na nzito.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005