o-AMINOPHENOL ICSC: 0824
Novemba 1998

2-Aminophenol
2-Amino-1-hydroxybenzene
o-Hydroxyaniline
CAS # 95-55-6 C6H7NO / C6H4(OH)(NH2)
RTECS # SJ4950000 Masi ya molekuli: 109.12
UN # 2512
EC # 612-033-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO

Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 20/22-40
S: (2-)-28-36/37
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 885
Msimbo wa NFPA: H 2; F 1; R 2;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
o-AMINOPHENOL ICSC: 0824
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ISO RANGI HADI NYEUPE. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA AU MWANGA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damukusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 170-174°C
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 1.7
Kiwango cha kumweka: 190°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.62
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Jotoridi linalosababisha mtengano haijulikani katika maandiko. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005