VINYL CYCLOHEXENE DIOXIDE ICSC: 0820
Novemba 1998

3-Oxiranyl-7-oxabicyclo4.1.0
1-Epoxyethyl-3,4-epoxycyclohexane
Vinyl cyclohexene diepoxide
CAS # 106-87-6 C8H12O2
RTECS # RN8640000 Masi ya molekuli: 140.2
UN # 2810
EC # 603-066-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na asidi na besi.


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa. Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu. Kuvimba.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/24/25-40
S: (1/2-)-23-24-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G06b
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, alkoholi, amini na misombo mingine ya hidrojeni zenye wepesi wa kumenyuka. Kavu. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
VINYL CYCLOHEXENE DIOXIDE ICSC: 0820
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha pamoja na asidi na besi kwa athari ya moto au mlipuko. Inapowaka hutengeneza moshi wa akridi na mafusho yakerayo. Humenyuka pamoja na misombo ya hidrojeni zenye wepesi wa kumenyuka (alkoholi, amini).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm; (kama TWA) (ngozi) (ACGIH 1998)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo, ovari, makende kusababisha vidonda vya tishu. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 227°C
Kiwango myeyuko: <-55°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.10
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 18.3
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: <0.13
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.8
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1
Kiwango cha kumweka: 110°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 393°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.3
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. EP-206, ERLA-2270, ERLA-2271, UNOX Epoxide 206, NCI-C60135, Chissonox-206 ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005