| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na halojeni, misombo ya halojeni na vioksidishaji.
|
Dioksidi kaboni, poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 30°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 30°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kichefuchefu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Degedege. Kupoteza fahamu. Udhaifu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2 Jasara tanzu za UN: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 42G11 Msimbo wa NFPA: H 4; F 4; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho, halojeni. Baridi. Kavu. Mahali kuna nitrojeni.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana kwa upole inapokanzwa ifikapo 150°C kutoa boroni na gesi inayoweza kuwaka (hidrojeni - tazama ICSC 0001), na inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za boroni). Humenyuka pamoja na halojeni, misombo ya halojeni, mafuta na grisi, na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Nyenzo isiyomenyu hushika moto kwa hewa bila kuwashwa. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.005 ppm; 0.013 mg/m³ (kama TWA); 0.015 ppm; 0.039 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1998) MAK: 0.005 ppm; 0.013 mg/m³ (1998) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini kusababisha degedege, kilicho na asidi na kuharibika kwa ini. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 60°C Kiwango myeyuko: -47°C Uzito wiani (maji = 1): 0.6 Umumunyifu katika maji: mmenyuko Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 22.8 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.2 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.3 Kiwango cha kumweka: 30°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: takribani 35°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.42-98 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile haloni. Dalili za madhara hazijitokezi mpaka baada ya masaa 48 kupita. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||