OXYGEN DIFLUORIDE ICSC: 0818
Novemba 1998

Oxygen fluoride
Fluorine monoxide
Difluoride monoxide
(silinda)
CAS # 7783-41-7 OF2
RTECS # RS2100000 Masi ya molekuli: 54.0
UN # 2190
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.

Moto unapotokea katika eneo: mioto mikubwa: mnyunyizio wa maji; mioto midogo: poda.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko. Kwa maji au mvuke inapasuka kwa nguvu ikiwashwa.

Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Upofu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 5.1 na 8

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
OXYGEN DIFLUORIDE ICSC: 0818
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI ILIYOBANWA YENYE HARUFU TAMBULISHI. IKIWA KAMA MAJI HUWA MANJANO-UTURUNGI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 250°C huzalisha gesi zenye sumu na babuzi. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka pamoja na iso-metali kama vile fosforasi nyekundu, poda ya boroni, na nyenzo yenye vinyweleo kama silika na alumina. Humenyuka kwa mlipuko kwenye joto la kawaida pamoja na sulfidi hidrojeni, pamoja na klorini, bromini au iodini kutokana na kupata joto kusababisha athari ya moto na mlipuko. Yapasuka ikigusa mvuke.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm; 0.11 mg/m³ (viwango vya juu kabisa) (ACGIH 1997)
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Mfiduo juu kidogo ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -145°C
Kiwango myeyuko: -224°C
Umumunyifu katika maji, ml/100 ml ifikapo 0°C: 6.8 (mmenyuko kwa upole)
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.8
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Uzito wa kioevu kwenye kiwango mchemko: 1.90 kg/l. Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005