MESITYL OXIDE ICSC: 0814
Machi 1998

4-Methyl-3-penten-2-one
Methyl isobutenyl ketone
CAS # 141-79-7 C6H10O / (CH3)2C=CH-COCH3
RTECS # SB4200000 Masi ya molekuli: 98.1
UN # 1229
EC # 606-009-00-1
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 25°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 25°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu. Maumivu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-20/21/22
S: (2-)-25
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 130
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
MESITYL OXIDE ICSC: 0814
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI KINATACHO CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUWA NYEUSI IKISIMAMO KWA MDA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Hushambulia plastiki nyingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 15 ppm; 60 mg/m³ (kama TWA);
25 ppm; 100 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kupoteza fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini, mafigo na mapafu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 130°C
Kiwango myeyuko: -41.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.865
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 3.3 (wastani)
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03
Kiwango cha kumweka: 25°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 340°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-7.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.7
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Viwango myeyuko vinginevyo: -59°C. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005