| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usiwashe moto.
|
Gesi ajizi, poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine. USITUMIE vitenzi vya majimaji.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kichefuchefu. Kutapika. Kuchanganyikiwa. Kupumua kwa shida. Mchomo. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge. Maumivu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Kuungua kunakopenya sana. Maumivu. Kiwaa.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kizunguzungu. Kuhara. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Mshtuko au kuzimia. Kutetemeka. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kisichoingiza hewa. Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43G04 Msimbo wa NFPA : H 3; F 4; R 2; W |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kavu. Weka katika gesi ajizi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO NYEUPE HADI KIJIVU, RISHAI KATIKA MAUMBO MBALIMBALI. ISO HARUFU. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA MWANGA. HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kuwaka papo hapo inapogusana na hewa. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikaboni vya halojeni, asidi na maji, kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001) Mmumunyo katika maji, hidroksidi lithiamu, ni besi kali. Inapogusana na nyuso zenye joto au mialimoto dutu hii hutengana na kutengeneza mafusho yanayokereketa ya alkali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.025 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1999). MAK: ppm; 0.025 mg/m³; (1999) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya erosoli kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango mchemko ifikapo 850°C Kiwango myeyuko: 680°C Uzito wiani (maji = 1): 0.76-0.77 Umumunyifu katika maji: mmenyuko |
Jotoridi la kujiwasha: 200°C | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji, dioksidi kaboni, povu au misombo halojeni kama vile tetra-kloridi kaboni. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||