KETENE ICSC: 0812
Oktoba 1997

Carbomethene
Ethenone
Ketoethylene
CAS # 463-51-4 C2H2O / CH2=C=O
RTECS # OA7700000 Masi ya molekuli: 42.0
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, dioksidi kaboni. USITUMIE maji.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Dutu haiwesi kuhifadhiwa au kupelekwa kwa meli.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
KETENE ICSC: 0812
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha kirahisi. Humenyuka vikali ikiwa na misombo kikaboni mingi. Humenyuka pamoja na maji kufanyiza asidi acetiki. Dutu hii hutengana pamoja na alkoholi na amonia.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 ppm; 0.86 mg/m³ (kama TWA);
1.5 ppm; 2.6 mg/m³ (kama STEL) (ACGIH 1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kusababisha kuvimba kwa mapafu na kua fuwele (emphesema, fibrosis).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -56°C
Kiwango myeyuko: -150°C
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.4
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005