ZINC CHROMATE ICSC: 0811
Aprili 2000

Chromium zinc oxide
Zinc tetraoxychromate
Chromic acid, zinc salt (1:1)
CAS # 13530-65-9 ZnCrO4
RTECS # GB3290000 Masi ya molekuli: 181.4
UN # 3288
EC # 024-007-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-22-43-50/53
S: 53-45-60-61
Angalia: [A; E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: <<23503160\6.1>>
Kikundi Ufungashaji cha UN: <<23505020\II>>
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G64b
Kilichofungwa vizuri. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ZINC CHROMATE ICSC: 0811
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA FUWELE MANJANO

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kam Cr): 0.01 mg/m³ (kama TWA) A1 (ACGIH 1999).
Ainisho ya MAK III.1.Sh (1999)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Kuvuta pumzidust kunaweza kusababisha kuwasha.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu waweza kusababisha vidonda puani. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 316°C
Uzito wiani: 3.4 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Jina la kromati zinki hutumika pia kumaanisha zinki nyingine za kiteknikali na kromati za zinki potasiamu. ZnCrO4.Zn(OH)2 inahusu nambari ya CAS 49663-84-5. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Pigment Yellow 36 na Buttercup Yellow ni majina ya kibiashara. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005