PROPIONIC ACID ICSC: 0806
Oktoba 1997

Ethylformic acid
Methylacetic acid
Propanoic acid
Ethanecarboxylic acid
CAS # 79-09-4 C3H6O2 / CH3CH2COOH
RTECS # UE5950000 Masi ya molekuli: 74.1
UN # 1848
EC # 607-089-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 54°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 54°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.> Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia. Kuumwa koo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 34
S: (1/2-)-23-36-45
Angalia: [B]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 642
Msimbo wa NFPA : H 3; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PROPIONIC ACID ICSC: 0806
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI KAMA MAFUTA, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni asidi kali ya kati. Humenyuka pamoja na besi, vioksidishaji vikali na amini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC0001).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm; 30 mg/m³ (ACGIH 1997).
MAK: 10 ppm; 30 mg/m³; (1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 141°C
Kiwango myeyuko: -21°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.99
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 390
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.6
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 54°C c.c. 57°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 485°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.1-12
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.33
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Luprosil, Prozoin, Tenox P Grain Preservative na Tenox P ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005