| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Mnyunyizo wa maji, poda.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji vikali.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. (Tazama Kumeza).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuvimba kwa kope za macho. Kiwaa. Upofu, hasa wa kudumu.
|
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Degedege. Kusinzia. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kutapika. Udhaifu.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 23/24/25-43-50/53 S: (1/2-)-28-36/37-45-60/61 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b
|
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, anhidridi asidi, vyakula na malisho. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEUPE HADI NYEKUNDU ISIYOKOZA. HUGEUKA GIZA INAPOFIDULIWA NA HEWA. HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Dutu hii ni kinakisishaji kikali na humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji na besi kali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 mg/m³ A4 (kama TWA) (ACGIH 1997) MAK: 0.1 mg/m³ H, S, IIIB (1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C; wakati wa kunyunyiza au kutawanya, hata hivyo, kwa kasi zaidi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho. Kuvuta pumzi yenye vumbi hili kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). Kuvimba kwa mdomo na koo yaweza kuonekana kufuatiwa kumezwa. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. Dutu hii huweza kuathiri mafigo kusababisha kuharibika kwa figo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 267°C Kiwango myeyuko: 139-147°C Uzito wiani (maji = 1): 1.1 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 4 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 100°C: 144 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Kiwango cha kumweka: 156°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 400°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.5-? | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Uhusiano baina ya harufu na kikomo cha mfiduo wa kazi hauwezi kuonyeshwa. Suuza nguo zilizosibikwa (hatari ya moto) kwa maji mengi. Benzofur D, Developer PF, Fourine D, Pelagon D, Orsin, Ursol-D na Vulkanox 4020 ni majina ya kibiashara.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||