4-NITRO-N-PHENYLBENZENAMINE ICSC: 0804
Oktoba 1999

4-Nitrodiphenylamine
p-Nitrodiphenylamine
p-Nitrophenylphenylamine
4-Nitro-N-phenylaniline
CAS # 836-30-6 C12H10N2O2 / C6H5(NH)C6H4(NO2)
RTECS # JJ9600000 Masi ya molekuli: 214.2
UN # 1325
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41G10
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali. Baridi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
4-NITRO-N-PHENYLBENZENAMINE ICSC: 0804
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO, KAMA SINDANO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za nitrojeni). Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 343°C
Kiwango myeyuko: 132-135°C
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: sio na maana
Kiwango cha kumweka: 190°C o.c.
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.82
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira. Dutu hii inaweza kusababisha madhara yatakayoonekana baadaye katika mazingira ya maji.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005