| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Mnyunyizo wa maji, povu linalokinza alkoholi, dioksidi kaboni, USITUMIE poda.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. (Tazama Vidokezo).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kutoa machozi. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Mchomo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: Xn R: 22-36/37/38-42 S: (2-)-22-28-39 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 824 Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 1; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO RANGI AU NYEUPE, YENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.25 ppm; 1.0 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1997). MAK: 0.1 ppm; 0.4 mg/m³; (1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera vibaya sana macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 202°C Kiwango myeyuko: 53°C Uzito wiani (maji = 1): 1.5 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 40 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 25 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4 |
Kiwango cha kumweka: 102°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 477°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.4-7.1 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile poda. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Husafirishwa pia ikiwa kioevu cha moto (70°C); kugusana na ngozi lazima kuepukwe. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||