FURFURYL ALCOHOL ICSC: 0794
Oktoba 1997

2-Furanmethanol
2-Furancarbinol
2-Hydroxymethylfuran
Furfural alcohol
CAS # 98-00-0 C5H6O2
RTECS # LU9100000 Masi ya molekuli: 98.1
UN # 2874
EC # 603-018-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 65°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 65°C, uingizaji hewa.

MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 20/21/22
S: (2-)
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G61c
Msimbo wa NFPA : H 1; F 2; R 1;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
FURFURYL ALCOHOL ICSC: 0794
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA NYEKUNDU AU KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA MWANGA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hupolimisha kwa kuathiriwa na asidi. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali au asidi kali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm; 40 mg/m³ (kama TWA),
15 ppm; 60 mg/m³ kama (STEL) (ngozi) (ACGIH 1997).
MAK: 10 ppm; 40 mg/m³; (1996).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo juu zaidi ya OEL husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 170°C
Kiwango myeyuko: -15°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.13
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 53
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 65°C c.c. 75°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 491°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-16.3
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.28
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Viwango myeyuko vinginevyo: -31°C. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005