CHLORMEQUAT CHLORIDE ICSC: 0781
Aprili 2000

(2-Chloroethyl)trimethylammonium chloride
2-Chloro-N,N,N-trimethylethanaminium chloride
Chlorocholine chloride
CAS # 999-81-5 (ClCH2CH2N(CH3)3)Cl / C5H13Cl2N
RTECS # BP5250000 Masi ya molekuli: 158.1
UN #
EC # 007-003-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MFIDUO KWA VIJANA NA WATOTO!

Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA!
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Utokaji mate kwa wingi. Kutokwa jasho. Kuona maruweruwe. Kuhara. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 21/22
S: (2-)-36/37
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri. Yaweza kuhifadhiwa kwenye vyombo vya kioo, plastiki nzito, mpira au vyombo vya metali iliyokingwa kwa utomvu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CHLORMEQUAT CHLORIDE ICSC: 0781
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE RISHAI, ISO RANGI HADI NYEUPE, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni. Dutu hii hutengana inapokanzwa kwa besi kali ya mmumunyo wa majimaji huzalisha trimetiliamini na mafusho. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Erosoli hii inakera kidogo macho. Dutu hii huweza kuathiri neva bila kuharibu shuguli za neva (cholinergic symptoms without acetylcholinesterase inhibition) (tazama Vidokezo).

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko (hutengana): 245°C
Umumunyifu katika maji: vizuri (74 g/100 ml ifikapo 20°C)
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Utumishi wa atropini kwa kutibu hauruhisiwi. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005