p-BENZOQUINONE ICSC: 0779
Oktoba 1997

2,5-Cyclohexadiene-1,4-dione
Quinone
1,4-Benzoquinone
p-Quinone
CAS # 106-51-4 C6H4O2
RTECS # DK2625000 Masi ya molekuli: 108.1
UN # 2587
EC # 606-013-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Mnyunyizio wa maji, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 38°C. Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Kugeuka rangi. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Rangi ya ukhanga.
Miwani ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/25-36/37/38
S: (1/2-)-26-28-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 1;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Baridi. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
p-BENZOQUINONE ICSC: 0779
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO YENYE HARUFU KALI. YAWEZA KUYEYUKA (SUBLIMSHA) HATA KWA JOTO YA KADIRI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. Iwapo kavu, huweza kuchajiwa kiumemetuamo kwa kuzinga, upitishaji nyumatiki, umiminaji, nk.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapopata joto zaidi ya 60°C, pamoja na unyevu, huzalisha monoksidi kaboni. Dutu hii ni kioksidishaji dhaifu, humenyuka vikali ikiwa na baadhi ya dutu zinazoweza kuwaka, kinakisishaji kikali na besi kali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm; 0.44 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1997)
MAK: 0.1 ppm; 0.4 mg/m³ (1997)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri macho. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kuleta kushinda kupumua na kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ngozi na macho kusababisha kukeuga rangi, kichomi na kuumiswa kwa konea (injury of the corneal epithelium).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: takribani 180°C
Kiwango myeyuko: 116°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.3
Umumunyifu katika maji: mbaya
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 12
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.0
Kiwango cha kumweka: 38-93°C
Jotoridi la kujiwasha: 560°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.2
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Maumbile hutegemea kuweko kwa mvuke hewani. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005