| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Silinda inaweza kulipuka kwenye joto la moto. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na ozoni au asidi nitriki iliyokolea.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Udhaifu. Mapigo moyo dhaifu na yasio na urari. Kukojoa damu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: Xn R: 20/22 S: (2-) Angalia: [A] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G43 Msimbo wa NFPA : H 4; F 4; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Baridi.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI ISO RANGI, ILIYOBANWA, YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana polepole kwenye joto la kawaida lakini haraka ifikapo 200°C huzalisha metali ya antimoni na hidrojeni. Humenyuka vikali ikiwa na klorini, asidi nitriki iliyokolea na ozoni kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.1 ppm; 0.51 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1997) MAK: 0.1 ppm; 0.5 mg/m³ (1996) |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu (haemolysis), mafigo, ini na mfumo mkuu wa neva. Mfiduo zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -18°C Kiwango myeyuko: -88°C Uzito wiani (maji = 1): 2.26 ifikapo -25°C Umumunyifu katika maji: mbaya Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.4 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Vikomo vya ulipukaji havijulikani katika maandiko, japokuwa dutu hii inaweza kuwaka na ina kiwango cha kumweka pungufu ya 61°C. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Uhusiano baina ya harufu na kikomo cha mfiduo wa kazi hauwezi kuonyeshwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||