ANTIMONY ICSC: 0775
Oktoba 1997

Antimony black
Antimony regulus
Stibium
CAS # 7440-36-0 Sb
RTECS # CC4025000 Masi ya atomi: 121.8
UN # 2871
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani. Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vioksidishaji vikali.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kutapika. (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kutapika. Kifo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G11c
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ANTIMONY ICSC: 0775
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
METALI SHEUPE KAMA FEDHA, ANGAVU, NGUMU, INAYOVUNJIKA HARAKA AU PODA YA RANGI YA KIJIVU.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu (oksidi za antimoni). Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji (e.g. halojeni, parmanganati alkali, nitrati), na poda za metali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka na asidi kutengeneza gesi (stibine) yenye sumu kali sana (tazama ICSC 0776).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV (kama Sb): 0.5 mg/m³ (kama TWA) (ACGIH 1997)
MAK kama Sb: 0.5 mg/m³ (1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mfiduo kwa kumeza huweza kusababisha mkereketo wa njia ya utumbo. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi hasa iwapo kuna mfiduo wa mvuke. Dutu hii huweza kuathiri macho, njia ya upumuaji na mapafu kusababisha ugonjwa wa mapafu unaotokana na antimoni (pneumoconiosis).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1635°C
Kiwango myeyuko: 630°C
Uzito wiani (maji = 1): 6.7
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 886°C: 133
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Viwango mchemko vinginevyo: 1325°C, 1440°C, 1750°C. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005