DIPHENAMID ICSC: 0763
Aprili 1997

2,2-Diphenyl-N,N-dimethylacetamide
N,N-Dimethyldiphenylacetamide
CAS # 957-51-7 C16H17NO
RTECS # AB8050000 Masi ya molekuli: 239.3
UN #
EC # 616-007-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi
Mtambo wa kutolea nje.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi

Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-52/53
S: (2)-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Kinachotenganishwa na asidi kali, besi na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIPHENAMID ICSC: 0763
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO NYEUPE KATIKA MAUMBO MBALIMBALI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa ifikapo 210°C na inapochomwa kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi pamoja na oksidi za nitrojeni. Humenyuka besi, asidi kali, vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaokera unaweza kufikiwa haraka.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 135°C
Uzito wiani: 1.2 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 27°C: 0.03
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.17
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. L 34314, Dymid, Enide ni majina ya kibiashara.
The cards has been partly updated in April 2005. See sections Environmental Data, EU classification.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005