4-AMINOBIPHENYL ICSC: 0759
Aprili 1997

(1,1'-Biphenyl)-4-amine
p-Biphenylamine
p-Xenylamine
4-Aminodiphenyl
CAS # 92-67-1 C12H11N / C6H5-C6H4NH2
RTECS # DU8925000 Masi ya molekuli: 169.2
UN #
EC # 612-072-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Mazimbwezimbwe. Kuumwa kichwa.
Mfumo funge na uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vinavyokalafatika; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b
Msimbo wa NFPA: H 2; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
4-AMINOBIPHENYL ICSC: 0759
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO ISO RANGI KATIKA MAUMBO MBALIMBALI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA ZAMBARAU INAPOFIDULIWA NA HEWA.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi zenye sumu. Mmumunyo huu katika maji ni besi dhaifu. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: A1 (ngozi) (ACGIH 1996)
Ainisho ya MAK: III A1 (1995)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri kibofu kusababisha damu kwa makajoo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 302°C
Kiwango myeyuko: 53°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.2
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.8
Kiwango cha kumweka: 153°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 450°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.8
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Unchunguzi wa kunatibabu unatakikana kwa muda fulani. Uangalifu wa kipekee unatakikana kwa masimbi ya makajoo na saitologia. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005