METHYLARSONIC ACID ICSC: 0755
Aprili 2005

Methanearsonic acid
Monomethylarsinic acid
MMA
Monomethylarsonate
CAS # 124-58-3 CH3AsO(OH)2 / CH5AsO3
RTECS # PA1575000 Masi ya molekuli: 140
UN # 1557
EC # 033-002-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-50/53
S: (1/2-)-20/21-28-45-60-61
Angalia: [A, 1]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-1
Kinachotenganishwa na besi kali, vyakula na malisho. Kavu. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYLARSONIC ACID ICSC: 0755
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO NYEUPE YA RISHAI KATIKA MAUMBO MBALIMBALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yenye sumu (oksidi za arseniki - tazama ICSC 0378). Mmumunyo huu katika maji ni asidi kali ya kati.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: BEI imetolewa; (ACGIH 2005).
MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa upole macho, ngozi na njia ya upumuaji. Ikimezwa mfiduo huweza kuleta uvimbe wa tumbo na chango (gastroenteritis). Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo na ini kusababisha kuharibika kwa utendaji. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 161°C
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu monosodium methanarsonate na disodium methanarsonate..
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005