| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!).
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: Xi R: 37-43 S: (2-)-8-24/25-46 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 4.2 Jasara tanzu za UN: 4.3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 42S2210
|
Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na asidi, vyakula na malisho. Kavu. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA KIJIVU-MANJANO HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana polepole inapokanzwa au inapogusana na asidi na unyevu huzalisha mafusho yakerayo na yenye sumu pamoja na oksidi za sulfuri, oksidi za nitrojeni, oksidi zinki, oksidi manganisi, sulfidi hidrojeni, sulfidi kaboni, ethylene thiuram sulfide, ethylene bisisothiocyanate, ethylene urea na 2-mercaptoimidazoline. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji, na inakera kwa upole ngozi. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana kabla ya kuyeyuka Uzito wiani (maji = 1): 1.92 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: sio na maana |
Kiwango cha kumweka: 138°C o.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.33 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii huingia katika mazingira kwa matumizi ya kawaida. Utaratibu wa hali ya juu lazima unahitajika ili kuzuia kiasi zaidi kisitokee kama kupitia kwa kutupwa ovyo.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Maneb, dutu inayohusika, huweza pia kusababisha madhara mengine baada ya kuwa katika mazingira yaliyo na dutu kwa muda mrefua. Angalia pia kadi ya viyeyusho endapo vimetumiwa kutengenezea dutu hii. Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini. Aimcozeb, Crittox MZ, Dithane 945, Dithane M-45, Fore, Karamate, Mancozin, Manzate 200, Manzin, Nemispor, Penncozeb, Phytox MZ, Riozeb, Vondozeb Plus ni majina ya kibiashara. Tazama ICSC 1148, 2-Mercaptoimidazoline, bidhaa chafuzi na inayovunjika, ICSC0173 Maneb na ICSC0350 Zineb.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||